NA TIGANYA VINCENT
HALMASHAURI ya Wilaya ya Tabora (Uyui) imetoa mikopo ya jumla ya shilingi milioni 43 kwa vikundi 13 kwa ajili ya kujiongezea kipato na kuondokana na umaskini.
Mikopo hiyo imekabidhiwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri kwa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Hemed Magaro alisema mikopo hiyo imetolewa kwa vikundi 6 vya wanawake ambavyo vimekopeshwa shilingi milioni 19, vikundi 6 vya vijana vimekabidhiwa shilingi milioni 19 na kikundi kimoja cha walemavu kimekabidhiwa shilingi milioni 5.
Amesema mikopo hiyo itavisaidia vikundi hivyo kuchangia katika kukuza uchumi kupitia uzalishaji wa mali.
Mwisho
Uyui District Council
Anuani ya Posta: S.L.P 610
Simu ya Mezani: +255 26 296 6008
Simu ya Mkononi: +255 766616985
Barua pepe: ded@uyuidc.go.tz
Copyright ©2016 UyuiDC . All rights reserved.