Mifugo na Uvuvi
UTANGULIZI:
Mifugo na Uvuvi inaundwa na Sehemu kuu mbili ambazo ni:-
(i) Mifugo
(ii) Uvuvi.
MAJUKUMU YA IDARA YA MIFUGO NA UVUVI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA TABORA.
Jukumu la Idara hii ni kutekeleza shughuli mbalimbali zinazohusiana na maendeleo ya mifugo na uvuvi kwa kushirikiana na Serikali kuu na Wadau kutoka Sekta binafsi. Shughuli zinazofanywa na Idara ni pamoja na:-
1. Maendeleo ya Mifugo
Kusimamia utekelezaji wa shughuli za Maendeleo ya mifugo na ufugaji kupitia huduma za ugani ikiwa ni pamoja na kuhamasisha uundwaji wa vikundi vya wafugaji. Kusimamia na kuratibu huduma za kinga na tiba kwa mifugo zitolewazo na Halmashauri ya Wilaya, Serikali Kuu na sekta binafsi. Kusimamia ukaguzi wa nyama na mazao yatokanayo na Mifugo. Kusimamia utoaji wa vibali mbali mbali vya kusafirishia mifugo na Mazao ya Mifugo ndani ya nchi na kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na serikali kuu yanayotokana na mifugo na mazao yake.
2. Uvuvi
Kusimamia shughuli za uvuvi ikiwa ni pamoja na kutoa leseni za uvuvi, kusajiri vyombo vya uvuvi, Kuhamasisha ufugaji wa samaki katika mabwawa kwa lengo la kuinua kipato na lishe, kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri yanayotokana na uvuvi,
HUDUMA ZITOLEWAZO NA IDARA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA TABORA.
1. Utoaji wa vibali vya kusafirisha mifugo ndani na nje ya Wilaya ya Tabora
- Ng’ombe/mbuzi na kuku.
Mfugaji au mtu yeyote anayehitaji kibali cha kusafirisha mifugo yake ndani ya Wilaya au nje ya Wilaya ya Tabora ni sharti atimize masharti yafuatayo ili aweze kupata kibali hicho
Uyui District Council
Anuani ya Posta: S.L.P 610
Simu ya Mezani: +255 26 296 6008
Simu ya Mkononi: (1) +255 768867886
Barua pepe: ded@uyuidc.go.tz
Copyright ©2016 UyuiDC . All rights reserved.