1.0 UTANGULIZI:
Ufugaji wa nyuki unafanyika kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Ufugaji Nyuki ya Machi, 1998, Sheria ya Ufugaji Nyuki Na. 15 ya mwaka 2002 na Kanuni za Ufugaji Nyuki, 2005. Sera ya Taifa ya Ufugaji Nyuki ya Machi, 1998 imelenga mambo makuu matatu ambayo ni:- (i) kukuza uchumi wa taifa (ii) kuhifadhi mazingira (iii) manufaa ya kijamii.
2.0 FAIDA ZA UFUGAJI NYUKI
3.0 MAJUKUMU YA KITENGO CHA UFUGAJI NYUKI
3.1 Elimu inayotolewa
Elimu inayotolewa inahusu yafuatayo:-
(i) Nyuki na tabia zake
(ii) Matumizi ya zana za ufugaji nyuki
(iii) Uanzishaji na usimamizi wa manzuki
(iv) Mizinga ya nyuki ya kisasa
(v) Uambikaji,utundikaji na ukamataji wa makundi ya nyuki
(vi) Uangalizi wa makundi
(vii) Mazao ya nyuki
(viii) Maadui wa nyuki na njia za kuwakabili
(ix) Uchakataji na ufungashaji asali na nta
(x) Sera, sheria na kanuni za ufugaji nyuki
(xi) Elimu ya ujasiliamali
4.0 IDADI YA WAFUGAJI
Baadhi ya wananchi katika Kata 30 hujishughulisha na shughuli za ufugaji nyuki kama inavyoonekana katika jedwali hapo chini.
Jedwali Na. 1
Mwaka
|
Idadi ya mizinga
|
Idadi ya wafugaji
|
Idadi ya uzalishaji
|
|||||||
Ya magogo
|
Ya magome
|
Ya kisasa
|
Me
|
Ke
|
Jumla
|
Asali kgs
|
Thamani Tshs.
|
Nta kgs
|
Tahamani Tshs.
|
|
2014/15
|
486,487
|
21,105
|
2,465
|
11,860
|
238
|
12,098
|
35,160
|
87,900,000
|
11,590
|
104,310,000
|
2015/16
|
487,717
|
20,683
|
2,515
|
12,175
|
325
|
12,445
|
50,700
|
152,100,000
|
21,304
|
234,388,000
|
2016/17
|
488,936
|
20,170
|
2,860
|
12,253
|
343
|
12,541
|
40,350
|
148,084,506
|
5,475
|
65,700,000
|
lifuatalo ni jedwali linaloonyesha idadi ya hifadhi za nyuki, vyama vya msingi vya ushirika wa wafugaji na vikundi vya nyuki.
Jedwali No. 2
Idadi ya hifadhi za nyuki
|
Idadi ya vyama vya msingi vya Ushirika vya ufugaji Nyuki
|
Idadi ya vikundi ya ufugaji Nyuki
|
25 |
4 |
28 |
Kuunda kikundi:Unatakiwa kuzingatia yafuatayo:-
(i) Kikundi kiwe na katiba.
(ii) Kikundi kisajiliwe kwa Mkurugenzi Mtendaji (wasiliana na Afisa Mtendaji kuhusu taratibu za kusajili kikundi).
(iii) Wanakikundi wawe tayari kupewa mafunzo ya ufugaji bora wa nyuki na ujasiliamali. Mafunzo yatatolewa kwa siku na muda mtakaokubaliana na wataalam.
Ufugaji binafsi au kikundi kuanzishwa inabidi kuzingatia sana uwepo wa eneo la kufugia (Manzuki) .
5.0 MANZUKI
Eneo maalumu au shamba linalotumika kuhifadhi makundi ya nyuki yaliyopo ndani ya mizinga kwa malengo ya kuzalisha mazao ya nyuki.
Sifa za manzuki:
Eneo lifaalo kwa shughuli za ufugaji nyuki ni lazima liwe na sifa zifuatazo:
Uyui District Council
Anuani ya Posta: S.L.P 610
Simu ya Mezani: +255 26 296 6008
Simu ya Mkononi: (1) +255 768867886
Barua pepe: ded@uyuidc.go.tz
Copyright ©2016 UyuiDC . All rights reserved.