NA TIGANYA VINCENT
HALMASHAURI ya Wilaya ya Uyui imetuma barua ya pongeza kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia kiasi cha shilingi bilioni 3.6 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa vyumba 123 vya madarasa kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19 .
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Said Ntahondi kwa niaba wenzake alimkabidhi barua hiyo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani kwa ajili ya kumfikishia Rais Samia.
Alisema kwa kipindi kifupi cha uongozi wa Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia , Uyui imepata fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara.
Alisema kati ya fedha hizo shilingi bilioni 2.4 ni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya Sekondari na bilioni 1.1 kwa ajili ya vyumba vya madarasa katika Shule Shikizi.
Ntahondi alisema kuwa kiasi cha shilingi milioni 90 ni za ujenzi wa nyumba za watumishi wa sekta ya afya na milioni 14.1 kwa ajili ya fedha za ufuatiliaji.
Alisema watahakikisha watumia kiasi cha shilingi milioni 20 kukamilisha darasa moja kama walivyoekelezwa .
Ntahondi aliongeza hivi Madiwani na Watendaji wa Halmashauri hiyo wamejipanga kusimamia ili kuhakikisha fedha zinatumika kwa makusudio yalipangwa.
MAELEZO KATIKA PICHA.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Saidi Ntahondi akimkabidhi barua Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dk. Batilda Buriani kwa ajili ya kumfikishia Rais Samia Suluhu Hassan.
Uyui District Council
Anuani ya Posta: S.L.P 610
Simu ya Mezani: +255 26 296 6008
Simu ya Mkononi: (1) +255 768867886
Barua pepe: ded@uyuidc.go.tz
Copyright ©2016 UyuiDC . All rights reserved.