Vikundi 14 vya Wajasiriamali katika Halmashauri ya Wilaya ya Uyui vimepatiwa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 102.5 ikiwa ni sehemu ya asilimia 10 ya mapato ya ndani.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji Hemed Magaro wakati wa sherehe fupi ya kukabidhi mikopo hiyo kwa vikundi hivyo.
Alisema kati ya vikundi hivyo 9 ni vya wanawake ambavyo vimekopeshwa kiasi cha shilingi milioni 65 na vikundi 5 vya vijana vimekopeshwa shilingi milioni 37.5.
Magaro alisema hadi hivi sasa katika kipindi cha mwaka huu wa fedha wameshatoa kiasi cha shilingi milioni 85.6 ambayo ni sawa na asilimia 42 ya kiasi cha shilingi milioni 202.7 ambazo zinatakiwa kukopesha kwa vikundi vya walemavu, vijana na wanawake.
Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema kuna madeni ya jumla ya shilingi 170.9 zinadaiwa kwa wakopaji ambapo kati ya hizo vikundi vya wanawake vinadaiwa shilingi milioni 58.4, vijana wanadaiwa shilingi milioni 96.2 na watu wenye ulemavu wanadaiwa milioni 16.2.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati aliitaka Halmashauri hiyo kuanza utoaji wa mikopo ya fedha nyingi na vifaa na zana mbalimbali ambazo zitawasaidia wananchi kuanzisha viwanda vidogo.
“Ifikie kipindi muanze kutoa mashine ili wananchi waweze kuwa na miradi mikubwa ambayo itaharakisha maendeleo” alisema
Alisema hatua hiyo itawasaidia kuwepo na matokeo makubwa katika maisha ya wananchi kutokana na aina ya mikopo waliyokopeshwa.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wakopeshaji kurejesha mikopo ili iweze kuwasaidia wengine kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo.
Mwisho
MAELEZO YA PICHA
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati (katikati) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 102.5 kwa ajili ya mikopo kwa vikundi 14 ikiwa ni asilimia 10 inayotokana na mapato ya ndani.
Uyui District Council
Anuani ya Posta: S.L.P 610
Simu ya Mezani: +255 26 296 6008
Simu ya Mkononi: (1) +255 768867886
Barua pepe: ded@uyuidc.go.tz
Copyright ©2016 UyuiDC . All rights reserved.